Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imetoa mkopo kiasi cha shilingi Milioni mia moja kumi na moja(111,000,000) kwa vikundi vya wanawake, Vijana na Wenye ulemavu ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato yake ya ndani ili kutimiza takwa la kisheria la Serikali Ya Awamu ya tano la kuwakwamua kiuchumi wananchi wa Wilaya hiyo.
Kiasi cha fedha hizi kimegawanjwa kwa makundi mbalimbali ambapo vimefanya matumizi mbalimbali, vikundi vya vijana wamenunua vyombo vya usafiri pikipiki maarufu kama boda boda ambazo watazitumia kusafirisha abiria kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wanwake wameanzisha miradi mbalimbali kama ya ufugaji, uuzaji mazao ya viungo, ushonaji nguo, Utengenezaji wa Batiki na Sabuni.
Akizungumza na wajasiriamali, leo ijumaa tarehe 27/11/2020 katika ukumbi wa Walimu (CWT) Mbunge wa Jimbo la Muheza ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mhe, Hamisi Mohammed Mwinjuma(MWANA FA) amesema atahakikisha anasimamia mikopo hiyo kwa karibu sana kuhakikisha wanawake wanapata asilimia 4, vikundi vijana asilimia 4 na Wenye ulemavu wanapatiwa asilimia 2 ya mikopo hiyo.
“nitahakikisha mikopo hii haitolewi kwa upendeleo, kila kundi litapata mkopo kama linavyostahili kulingana na mwongozo wa Serikali” alisisitiza Mhe Mbunge.
Aliendelea kuwa pesa watakazopewa wanavikundi wakazitumie kwa shughuli za kikundi ili waweze kutekeleza malengo na kuboresha maisha yao wasizitumie kununulia matumizi ya nyumbani kwani watashindwa kurejesha
Katika hatua nyingine ameahidi kuweka mikakati ya kuongeza mapato ili kiwango cha mikopo kiweze kuongezeka na kusaidia wananchi wengi kwa wakati mmoja pia atahakikisha fedha hazirudishwi kwenye Halmashauri.
Awali akisoma taarifa ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu kwa kipindi cha mwezi julai hadi Novemba 2020 Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Muheza Vije Mfaume Ndwanga amesema katika kipindi hiki Halmashauri imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi Milioni mia moja kumi na moja(111,000,000) kwa vikundi 18 ikiwemo vya wanawake 10, vijana 7 na Wenye ulemavu 1.
Aliendelea kuwa vikundi hivyo vina jumla ya watu 175, wakiwemo wanawake 100, vijana 70, na watu wenye ulemavu 5 ambapo miongoni mwao wanaume wanne (4) na Mwanamke mmoja(1).
Aliongeza kuwa kwa kipindi cha mwaka 2020/2021 Halmashauri imetenga Shilingi 210,000,000/=ikiwa ni asilimia kumi ya makisio ya mapato ya ndani ambayo ni Shilingi 2,100,000,000 yenye lengo la kutoa mikopo kwa vikundi 42 vya uzalishaji mali vya wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu.
Nae Mkuu wa Usalama barabarani wa Wilaya ya Muheza Ndugu Richard Mmuwe amewataka vijana wa waendesha pikipiki (bodaboda) kuzingatia kanuni na sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali zinazoweza kuwavunja viungo vyao vya mwili, pamoja na faini na adhabu zilizowekwa kwa mamlaka Serikali. Pia amewataka wajiepushe na pombe kwani ndio inayowapelekea kupata ajali.
Kwa upande wa wanufaika wa mikopo wametoa shukrani kwa Serikali awamu ya tano inayoongozwa na DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, Mkuu wa Wilaya Muheza na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza kwa kuwaona na kuwapatia mikopo itakayowasaidia kuboresha maisha yao na kuahidi kurejesha mkopo kwa wakati.
Mbunge wa jimbo la Muheza Hamisi Mohammed Mwinjuma(MWANA FA) akizungumza kabla ya makabidhiano ya pikipiki yaliyofanyika leo ijumaa tarehe 27/11/2020 katika ukumbi wa CWT wilayani Muheza | Afisa maendeleo ya jamii Wilaya Muheza Vije Mfaume Ndwanga akizungumza kabla ya kukabidhi bodaboda za vikundi. |
|
|
|
|
||||
|
|
|||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.